Makumi kwa maelfu ya misikiti nchini Saudi Arabia imefunguliwa leo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili lakini waumini wameamriwa kuzingatia masharti makali ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Karibu misikiti 90,000 imeruhusiwa kuanza kutumika tena baada ya serikali nchini Saudi Arabia kukamilisha zoezi la kusafisha mazulia, vyoo na makabati yanayohifadhi kitabu kitukufu cha Quran.

Wizara inayoshughulikia masuala ya dini imetuma ujumbe mfupi kwa raia nchini humo kuwafahamisha kuhusu kanuni mpya za kushiriki ibada ikiwemo kuzingatia umbali wa mita mbili, kuvaa barakoa na kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono.

Katika hatua nyingine, mjini Jerusalem msikiti wa Al-Aqsa, ulio wa tatu kwa utukufu katika dini ya kiislamu pia umefunguliwa kwa mara ya kwanza tangu ulipofungwa katikati ya mwezi Machi kufuatia kusambaa kwa virusi vya corona.

The post Misikiti yafunguliwa Saudi Arabia, waumini wapewa kanuni mpya za kushiriki ibada appeared first on Bongo5.com.