Kada Mwingine wa Chama cha Mpinduzi ambaye alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha IFM Bwana Bakari Rashid Bakari amejitokeza katika Ofisi kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Mjini Unguja kwa lengo la kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM.Bwana Bakari Rashid Juma aliwasili katika ofisi za Chama hicho kisiwandui Mjini Unguja, majira ya saa sita za mchana huu na kuchukua fomu hiyo ambapo alikabidhiwa na Katibu wa Kamati Maalumu  ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.

Mara baada ya kuchukua fomu  Bwana Bakari alisema leo tarehe 22 Juni ameamua kujitokeza kuchukua fomu kwa lengo la kugombea nafasio ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi ccm.

“Mimi nataka kusema leo nimekuja kuchukua fomu sina mengi ya kuzungumza ila kadi ya chama cha mapinduzi nilikabidhiwa mwaka 1986 nikiwa na umri wa miaka 21 ambapo tokea hapo sikurudi nyuma.Aliongeza kusema amefundisha vyuo vingi sana Zanzibar na Tanzania bara pamoja na vyuo ambavyo vipo nje ya nchi kama vile afgnistan.

“leo sio siku ya kuongea sana nimekabidhiwa makaratasi mengi sana   na nina mchakato mkubwa wa kuatafuta wadhamini kwaiyo naiomba kwa leo muniache nikatafute hao wadhamini na harakati nyingine” alisema Bakari Rashid Bakari.

Hadi sasa jumla ya Mkada 21wamejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia tiketi ya chama hicho.