Mfalme Phillipe wa Ubelgiji ameelezea majuto yake kwa madhara yaliyosababishwa na ukoloni wa nchi yake nchini Kongo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa utawala wa Ubelgiji kutamka kauli kama hiyo.

Belgian king expresses 'deepest regrets' for colonial cruelties in ...

Katika barua yake aliyompelekea Rais Felix Tshisekedi hivi leo katika siku ambayo Kongo inaadhimisha miaka 60 ya kumalizika kwa ukoloni wa Ubelgiji, Mfalme Phillipe amesema anajutia majeraha ya kale ambayo maumivu yake yapo hadi leo kutokana na ubaguzi unaoendelea kwenye jamii.

Wanahistoria wanasema mamilioni ya Wakongo waliuawa, kukatwa viungo vyao ama kufa kwa maradhi wakati wakifanyishwa kazi kwenye mashamba ya mpira yaliyokuwa yakimilikiwa na Mfalme Leopold II wa Ubelgiji.

Philippe ascends to the throne of a divided Belgium, World News ...

Bila ya kumtaja babu yake huyo mkuu kwa jina, Mfalme Phillipe ameandika kwenye barua hiyo kwamba matendo ya ukatili na unyama yaliyofanywa wakati huo ni sehemu kubwa ya kumbukumbu za pamoja kati ya Kongo na Ubelgiji.

Masanamu kadhaa ya Leopold, aliyetawala baina ya mwaka 1865 na 1909, yamechafuliwa kwa rangi au kuvunjwa na waandamanaji nchini Ubelgiji katika siku za hivi karibuni, katika wimbi la hasira lililochochewa na mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd mwezi uliopita akiwa mikononi mwa polisi wa Minneapolis, Marekani.

The post Mfalme Phillipe wa Ubelgiji ajutia walichokifanya nchini Kongo appeared first on Bongo5.com.