MWANAMUZIKI anayefanya poa kwenye muziki wa Singeli Bongo, Khalid Sadick ‘Meja Kunta’, amefunguka juu ya kusikitishwa kwake na kile kilichotokea kwenye uchumba wa mwanadada mwigizaji wa Kibongo, Jacqueline Wolper na mbunifu wa mavazi, Rashid almaarufu kama Chid Designs.

 

Uchumba wa Wolper na jamaa huyo ndio habari ya mjini kufuatia kudumu kwa siku sita tu kabla ya kuvunjika.

Uchumba wa Wolper ndio unatajwa kushikilia rekodi ya kudumu kwa muda mfupi zaidi Bongo.

 

Katika mazungumzo yake na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Meja Kunta anayetajwa kuwa na ukaribu mkubwa na Wolper, amesema kuwa, amesikitika kutokana na ishu hiyo, kwani Wolper ni mtu wa karibu na amekuwa akisapoti kazi zake.

 

“Wolper ni mshkaji wangu sana, amekuwa akisapoti kazi zangu na sivyo watu walivyokuwa wakifikiria kuwa tuna uhusiano. Kama mshkaji, nimesikitika kutokana na ishu ambayo amekutana nayo