Rais Magufuli ni rais wa mfano sio Tanzania tua au Afrika ni dunia nzima, Wananchi wa Dodoma wamshukuru sana Rais Magufuli fursa zote zipo kwao.

Mwanasheria John Simon Kyashama ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la River of Healing Ministry lililoko kiluvya kwa komba ametoa maoni yake kuhusu Hotuba ya Rais Magufuli na kumpongeza kwa kile alichokifa ikiwemo kuzindua rasmi ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma na kuwakabidhi wastaafu Tausi.

 

mbali na kumpongeza rais Magufuli kyashama aetumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wa mkoa wa Dodoma kuitumia vizuri fursa waliyoipata ya kujengwa Ikulu Chamwino pamoja na wizara zote kuhamishiwa mkoani humo.

Kyashama ameongeza kuwa Rais Magufuli ameuonyesha ulimwengu kuwa yeye ni Rais wa dunia nzima sio tu Tanzania wala Afrika bali ni rais wa dunia nzima maana maono yake yamekuwa makubwa sana, Akitolea mfano sakata la Corona na namna ya uendeshaji wa nchi yake.

The post Mchungaji Kyashama: “Rais Magufuli ni Rais wa mfano na wa kuigwa dunia nzima sio Tanzania tu wala Afrika” – Audio appeared first on Bongo5.com.