Siku ya Jumatatu iliyopita usiku, George Floyd aliuawa baada ya afisa wa polisi wa mji wa Minneapolis kumkandamiza na goti shingoni kwa zaidi ya dakika nane, na kusababisha maandamano katika mji mbalimba baada ya video ikimuonyesha afisa huyo wa Polisi akitenda tukio hilo na mpaka hivi sasa maandamano yamechukua wiki nzima.

Mpaka hivi sasa inaelezwa ni zaidi ya miji 30 nchini Marekani na hata nje ya taifa hilo watu wameandamana kushinikiza hukumu juu ya afisa huyo wa Polisi alisababisha kifo kwa makusudi.

Mbali ya watu mbalimbali kuonyesha kuchukizwa na tukio hilo pia wachezaji wa mpira wa miguu wameonyesha kuchukizwa huku wengine wakitumia nafsai zao kukemea na kutaka haki itendeke.

Machezaji wa klabu ya PSG Kylin Mbappe ametumia ukurasa wake wa Instagram kukemea kwa kuandika “#JusticeForGeorge”.

Mbali na huyo pia mchezaji wa klabu ya Dortmund Jadon Sancho ametumia mchezo wa jana kati ya timu yake dhidi ya hammeringambapo timu yake ilishinda goli 6- na yeye akifunga goli tatu, aliamua kuonyesha t-shirt aliyokuwa ameivalia kwa ndani akishinikiza haki itendeke. lskini pia baada ya mchezo alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuandika ujumbe huu.

First professional hat trick A bittersweet moment personally as there are more important things going on in the world today that we must address and help make a change. We have to come together as one & fight for justice. We are stronger together!

#JusticeForGeorgeFloyd

Mbali na hao pia mchezaji w aklabu ya Weston McKennie Schalke 04 ya Ujerumani ambaye pia ni raia wa Marekani alilaani vikali pia alivaa kitamba wakati timu yake ikicheza kikisomeka Justice for Foyd na kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa.

To be able to use my platform to bring attention to a problem that has been going on to long feels good!!! We have to stand up for what we believe in and I believe that it is time that we are heard! #justiceforgeorgefloyd #saynotoracism

Mbali na hao pia mchezaji wa mpira wa kikapuanayekipiga katika timu ya Los Angeles Lakers Lebron Jmaes amtumia mitandao yake ya kijamii akilaani vikali kwa kuandika kuwa. “Why doesn’t America Love us……?”

Hao ni baadhi lakini wachezaji wengi sana ametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kulaani kitendo alichofanyiwa Mmarekani mweusi Flod na afisa wa Polisi.

The post Mbappe Lebron James, Sancho wapaza sauti kushinikiza haki itendeke kwa Polisi alimuua Mmarekani mweusi appeared first on Bongo5.com.