Mvutano kati ya mataifa makubwa yanayoshikilia uchumi wa Dunia, China na Marekani unaendelea kuwapo, ambapo hapo jana Jumatano utawala wa Rais Trump umeamuru kusitishwa kwa safari zote za ndege za mashirika ya ndege ya China kwenda na kutoka Marekani.
Wakati hayo yakijiri upande wa China hii leo imesema kuwa itaruhusu ndege za kigeni ambazo zimezuiwa hivi sasa kufanyakazi nchini humo kuanza safari za abiria kuanzia Juni 8, na kuondoa marufuku kwa ndege za Marekani.
Waandamanaji mjini Hong Kong
Wakati huo huo bunge la Hong Kong limepitisha sheria tata ya mswada wa wimbo wa taifa leo ambao utafanya kutoheshimu wimbo wa taifa wa China kuwa ni kosa la jinai, hatua ambayo wakosoaji wanaiona kuwa ishara ya hivi karibuni kabisa ya Beijing kukaza kamba katika mji huo. Uamuzi huo unaweza kuzusha maandamano zaidi katika mji huo.
The post Mashirika ya ndege China yapigwa ‘Stop’ Marekani, mvutano waendelea appeared first on Bongo5.com.