George Floyd, ambaye kifo chake huko Minneapolis wiki iliyopita kilisababisha maandamano makubwa juu ya udhalilishwaji wa watu weusi unaofanywa na polisi, alipatikana na virusi vya Corona wiki chache kabla ya kifo chake, ripoti ya uchunguzi wa mwili ya siku ya Jumatano imeonesha.

Hati yenye kurasa 20 iliyotolewa na Ofisi ya Uchunguzi wa Kitabibu ya Kaunti ya Hennepin imesema kuwa, vipimo vya COVID-19 vya Floyd vya mnamo Aprili 3 vilionesha uwepo wa maambukizi ya virusi hivyo, ripoti iliyotolewa kwa umma kwa ruhusa kutoka kwa familia ya Floyd.

Kwa sababu RNA ya kirusi yaweza kubaki katika mwili wa binadamu kwa wiki kadhaa baada ya ugonjwa kutoweka, kulingana na uchunguzi, kipimo cha mara ya pili kilichoonesha uwepo wa maambukizi baada ya kifo chake kilimaanisha kuwa Floyd, 46, alikuwa na maambukizi ya awali yasiyo na dalili alipofariki dunia mnamo Mei 25

The post Marekani: Vipimo vyaonesha George Floyd alikuwa na corona appeared first on Bongo5.com.