Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limekamata Bastola mbili na kuwaua majambazi wawili katika matukio mawili tofauti.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema mmoja wa majambazi ameuawa katika eneo la Mbagala Zakheim ambapo alikuwa na wenzake watatu wakijiandaa kuvamia maduka ya miamala ya fedha.

Jambazi wa pili aliuawa katika eneo la Shekilango baada ya majambazi kujaribu kuwashambulia askari waliokuwa doria wakiwafuatilia hivyo katika kujihami maaskari wakafanikiwa kumpiga risasi mgongoni.

Aidha Mambosasa ameeleza silaha walizozikamata ni Bastola mbili moja ikiwa na risasi tano huku ikiwa imetengezwa nchini Brazil.


Zaidi msikilize Kamanda hapo chini: