Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu amesema Sheria inampa uwezo wa kuwaondolea sifa wa kuendesha magari ya mizigo na biashara kwa miezi 6

Ameyasema hayo akiwa anazungumzia tukio la hivi karibuni la video iliyosambaa ikionyesha Mabasi ya kampuni ya Rungwe Express na Happy Nation yakishindana barabarani

Kamanda amesema, Madereva hao walikuwa wame-beti na tayari wote wamekatwa huku mmoja alikamatwa Dar es Salaam na mwingine Iringa

Aidha, amesema wanamtafuta mtu aliyekuwa anahamasisha tukio hilo. Amesema kwa mujibu wa Sheria 111 ya Sheria za usalama barabarani, sura ya 168 inasema yeyote atakayeonekana anahamasisha madereva kuvunja sheria, anavunja sheria