Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare amewataka wasomi wa CHADEMA kufanya tathmini ili kujua wanaongozwa na watu wa sampuli gani

Lwakatare ambaye alikuwa akihutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara jimboni kwake amesema "Viongozi wa CHADEMA ni kama vile wana maplastiki vichwani badala ya Ubongo"

Amewashangaa CHADEMA wanavyompinga Rais Magufuli kwa mambo makubwa ya ujenzi wa miundombinu aliyoyafanikisha wakati wao ukarabati wa jengo lao la Makao Makuu unawashinda ili hali wanapokea mabilioni ya shilingi kama ruzuku kila mwaka

Lwakatare alifukuzwa uanachama wa CHADEMA hivi karibuni baada ya kutotii agizo la Chama hicho la kutohudhuria Bunge kutokana na COVID19. Baada ya kufukuzwa alirejea na kujiunga na Chama cha CUF