Lazaro Nyalandu, ametangaza kutia nia ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku akibainisha vipaumbele 25 atakavyovifanya ndani ya siku 100 endapo atapewa ridhaa na Watanzania.

Nyalandu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) kanda ya Kati ametangaza nia hiyo Jumapili tarehe 14 Juni 2020 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Nyalandu amesema,  amemwandikia burua Katibu Mkuu  kumjulisha kusudio lake la kutia nia katika kinyang’anyiro cha kuwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA

“Nasimama mbele yenu na mbele ya umma wa Watanzania, huku moyo wangu ukiwa umejaa shauku kubwa nikitamani kuiona Tanzania, nchi tuipendayo kwa moyo wote inapata ustawi na kuendeleza matamanio, matarajiona ndotoza watu wake.

“Katika kuwapatia maendeleo endevu likiwa ni Taifa linalosimamia uhuru na  haki za watu, utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari,na demokrasia ya kweli inayowapa wananchi mamlaka ya juu kuhusu mustakadhi na mwelekeo ya nchi kupitia chaguzi zilizo huru na za haki,” amesema Nyalandu

==>>Msikilize hapo chini