Kauli za IGP Sirro zinamuelekeo na zinaviashiria kwa Jeshi la Polisi kuendelea k ( 344 X 640 ).jpg


Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika leo ametoa kauli kali ambayo ndio kauli halali ya Chama chake kuhusiana na Propaganda za kishamba zinazosambazwa na Jeshi la polisi zikiongozwa na IGP Sirro mwenyewe kuhusiana na shambulizi alilofanyiwa Mh Mbowe na Watu waliotumwa kumdhuru .

Hakuna ushahidi wowote kwamba Mbowe alilewa kama Sirro na waliomtuma wanavyoropoka mitaani , tarehe 8 na 9 June Mh Mbowe hakuwahi kukanyaga Royal Village Hotel kama watunga uongo wanavyodai , na kama kuna anayebisha alete ushahidi wa Mh Mbowe kuwepo eneo hilo kwa tarehe zilizotajwa kama waongo wanavyodai , Hakuna mtu yeyote kati ya wapiga kelele akiwemo Ndugai au Sirro wanaoweza kuthibitisha jambo hilo , wala hakuna Daktari hata mmoja katika waliomtibu Mbowe aliyethibitisha hilo , bali uongo huu unaosimamiwa na IGP kwa kulishwa maneno na Ndugai umeletwa makusudi kwa lengo la kuzima uchunguzi wa kuvamiwa kishamba kwa Mh Mbowe , kama Sirro ana ushahidi auweke hadharani .

Natoa wito kwa Chadema kumchukulia hatua IGP Sirro kwa kujiingiza kwenye siasa tena kwa kutumia Mguu wa kushoto , ikiwa Sirro anahitaji uongozi wa kisiasa basi amuombe Mwenyekiti wake wa ccm amruhusu ili tupambane naye majukwaani , Asijiingize bila taarifa ili asitumbuliwe .