Warusi wamepiga kwa kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, juu ya iwapo mchakato huo utamruhusu Rais Vladimir Putin kuwania mihula miwili zaidi madarakani, ambayo itambakisha madarakani hadi mwaka 2036.
Ingawa umaarufu wake umeporomoka kutokana na athari za janga la virusi vya corona, Putin mwenye umri wa miaka 67 bado anao uungwaji mkono mkubwa nchini Urusi.
Zoezi hili la kura ya maoni ambalo linatarajiwa kukamilika Jumatano ijayo, linatarajiwa kuidhinisha mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa na serikali ya Rais Putin.