Jeshi la Korea Kaskazini, limetishia kuingia tena, katika eneo lililoko kati yao na Korea Kusini, ambalo kwa mujibu wa makubaliano waliyosaini, halipaswi kuwa na shughuli za kijeshi.

North Korea Attacks Inter-Korean Liaison Office, South Korea Says ...

Kwenye taarifa ambayo imeripotiwa na shirika la habari la nchi hiyo (KCNA), na pia kunukuliwa na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, mkuu wa jeshi la Korea Kaskazini amesema wanafuatilia kwa karibu hali ya sasa, ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili, unazorota, na wanajiandaa kijeshi kwa hatua yoyote itakayoamuliwa na serikali.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Jeshi la Korea Kaskazini (KPA), linatathmini mpango wa kuwapeleka wanajeshi katika eneo hilo, ili kuimarisha ushikaji doria wa kijeshi dhidi ya Korea Kusini.

Tangazo hilo limejiri baada ya Korea Kaskazini kuthibitisha kuwa, iliripua ofisi ya pamoja kati yake na Kusini katika eneo hilo, kama hatua ya kuendelea kukata uhusiano wao na Kusini, ikiituhumu kusini kuruhusu kampeni ya propaganda dhidi ya kiongozi wake Kim Jong Un.

The post Korea Kaskazini wajiandaa, mkuu wa Jeshi asikilizia maamuzi ya serikali appeared first on Bongo5.com.