Mamia ya waombolezaji wameshiriki katika ibada ya kumkumbuka George Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyekufa mikononi mwa polisi wiki iliyopita katika jimbo la Minnesota.

Kiongozi wa kutetea haki za binadamu Al Sharpton ameapa kuwa maandaano makubwa yataendelea hadi watakapobadilisha mfumo mzima wa haki nchini humo.

Maandamano hayo, mengi yakiwa ya amani, yaliandaliwa kwa siku ya kumi mfululizo wakati wa usiku katika miji mbali mbali ikiwa ni pamoja na New York ambapo maelfu ya watu waliandamana huko Brooklyn Bridge pamoja na Washington, DC, Seattle na Los Angeles ambapo marufuku ya kutotoka nje imeondolewa.

Kifo cha Floyd kimechochea kuibuka upya kwa ghadhabu ya muda mrefu dhidi ya mauaji ya Wamarekani weusi mikononi mwa polisi na kusababisha wimbi la machafako ya kitaifa tofauti na lolote ambalo limewahi kushuhudiwa nchini Marekani tangu mauaji ya Martin Luther King ya mwaka 1968.

The post Kiongozi wa kutetea haki za binadamu aapa maandamano makubwa kuendelea Marekani appeared first on Bongo5.com.