Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesitisha mipango yake ya kijeshi ya kuchukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Korea Kusini.

Kim Jong-un - Family, Education & Facts - Biography

Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ililipua ofisi ya mawasiliano kati yake na Korea Kusini iliyoko katika upande wake wa mpaka na kutishia hatua za kijeshi zisizofahamika dhidi ya jirani yake huyo.

Korea Kaskazini ilikuwa inalenga kuiadhibu Korea Kusini kwa ukosefu wa maendeleo katika ushirikiano wa nchi hizo mbili na kushindwa kuwazuia wanaharakati kusambaza vijikaratasi vya propaganda dhidi ya Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini haikuweka wazi sababu ya uamuzi wake huo. Baada ya wiki kadhaa za kuchochea mivutano ya makusudi, inawezekana Korea Kaskazini inaipa muda Korea Kusini kuridhia masharti yake.

Imeandikwa na Hamza Fumo

The post Kim Jong Un aahirisha mipango yake ya kulipiza kisasi  appeared first on Bongo5.com.