Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi amesema kuwa lazima atatekeleza agizo alilopewa na Rais Magufuli haraka iwezekanavyo, lakini hawezi kurudiana na 'Ex' zake alioachana nao.


Kauli hiyo ameitoa leo Juni 18, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa upendo aliooneshwa na Rais Magufuli ni mkubwa hivyo hawezi kumuangusha, na kwamba anajipanga ili akutane na mke sahihi.

"Wachumba niliokuwa nao ni hao wawili kwa nyakati tofauti, sasa hivi tena inabidi nikae nijipange lakini agizo la Rais Magufuli nitalitekeleza haraka iwezekanavyo, ila nadhani tunaweza tukarejeana na Fatma Karume kwa sababu nasikia anataka kugombea Urais kupitia chama kile, pengine nikawa mume wa mgombe Urais" amesema DC Katambi.

Siku za hivi karibu Rais Magufuli aliwaagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi, waoe haraka kwa kuwa wanawake wazuri ni wengi na kwamba Jiji kama hilo haliwezi kuongozwa na watu ambao hawajaoa.