Msanii wa muziki wa Bongo Fleva @malkiakaren amefunguka mengi sana kuhusu maisha yake binafsi na maisha ya muziki. Akiongea na Bongo5 @malkiakaren amesema kuwa baada ya ile kauli ya baba yake kuwa anamuombea apate mwanaume aliyemzidi umri alitafutwa na wazee wengi sana akiwaita (MASHUGADADY) huku akiongeza kuwa kuna DM nyingi sana kwenye simu yake wanaume wakimtongoza.

@malkiakaren ameongeza kuwa Wanaume wanaomtafuta hawana pesa hivo yeye hawataki maana hawatakuwa na msaada kwake. “Mfano natakiwa nikashut nywele navaa ya milioni 2.5 halafu wewe huna hela nikikuomba na huna utajisikiaje? Kwahiyo mimi siwataki “

Mbali na hilo ametuma salama zake kwa @officialalikiba baada ya kuonyesha kuridhishwa na uandishi wake pia kwa kuimba wimbo wake. “Watu wengi baada ya kumuona @officialalikiba anaimba wimbo wangu wakaona kama @officialalikiba amemkubali sisi akina nani..? Aliniongeza mashabiki wengi sana na nilipata simu nyingi nikipongezwa “

The post Kareen “Baba yangu alipelekea nitafutwe na wazee wengi wakitaka kunioa, Kama Alikiba anaimba nyimbo zangu wengine akina nani” – Video appeared first on Bongo5.com.