Kampeni inayopigania kuchagliwa tena kwa Rais Donald Trump imepinga madai kwamba kampeni ya mitandao ya kijamii kwa njia ya Tik-Tok na K-Pop fans ndizo zilizosababisha kujitokeza kwa idadi ndogo ya watu katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi iliyofanyika Oklahoma Jumamosi usiku kuliko ilivyotarajiwa. 

Vijana wadogo wanasemekana kuwa walijiandikisha kununua tiketi wakiwa na nia ya kutohudhuria mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha viti vinabaki tupu katika mkutano huo. 

Lakini kikosi cha kampeni cha 2020 cha Trump 2020 kilisema kuwa kilikua kimeondoa tiketi hizo feki. 

Bwana Trump alisema kuwa Bwana Trump anatarajia watu milioni mojo kuja kwenye mkutano huo wa kampeni. 


Ilitarajiwa kuwa watu wangejaa hadi nje ya uwanja wa kituo hicho na mipango ikawekwa ili kuhakikisha watu wa ziada wanashiriki kikamilifu tukio hilo, lakini mipango hiyo ilifutwa kutokana na kwamba idadi viti vilibaki wazi. 

Kikosi cha zimamoto cha Tulsa kimenukuliwa kikisema kuwa zaidi ya viti 6,000 ndivyo vilivyokaliwa katika ukumbi huo, lakini kampeni ya Trump ilisema kuwa idadi ya waliohudhuria ilikua ni ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa kikosi cha kampeni ya Trump alisema katika taarifa aliyoitoa kuwa "maombi ya tiketi za simu hatukuyafikiria" kwani tuliwapokea watu kwa misingi ya Yule anayefika ndiye anayehudumiwa kwanza . 

Brad Parscale alivilaumu vyombo vya habari na waandamanaji kwa kuzishawishi familia zisihudhurie kampeni hiyo. 

"Watu wa itikadi za mrengo wa kushoto na kampeni za mtandao wanafanya kampeni, wakidhani kuwa kwa namna Fulani wataathiri mahudhurio ya mkutano wa kampeni, hawajui wanachokizungumzia au namna mikutano ya kampeni inavyofanyika ," Bwana Parscale alisema. 

"Kujisajiri kwa mkutano wa kampeni inamaanisha kuwa umethibitisha kuwa utahudhuria kwa namba ya simuna tunatoa mara kwa mara wajumbe gushi, kama tulivyowafanya maelfu katika mkutano wa Tulsa, kwa kuhesabu watu wenye uwezekano wa kuhudhuria ." 

Idadi kubwa ya wazazi walijibu ujumbe uliotumwa na Bwana Schmidt wakisema watoto wao walikua wamefanya sawa na hivyo. 

Alexandria Ocasio-Cortez, mtu maarufu, aliwasifu vijana na kampeni mtandao wa kijamii ta K-pop fans akisema kuwa walikua "wamefurika kampeni ya Trump na kujisajiri kwa tiketi gushi za kuhudhuria mkutano wa kampeni yake ". 

Haijawa wazi ni maelfu mangapi ya yaliyosajiliwa kuwa gushi na kikosi cha kampeni ya Trump, lakini video moja ya mtandao wa kijamii ya Tiktok kuanzia June iliwashawishi watu kujiandikisha kwa ajili ya kupata tiketi za bure ili kuhakikishakunakua na viti vitupu katika uwanja, imep