NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa mikopo ya shilingi milioni 332 kwa vikundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.

Mikopo hiyo imekabidhiwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mikopo hiyo , Mkurugenzi Mtendaji Dkt. John Pima alisema kati ya fedha shilingi milioni 215 kwa vikundi 38.

Alisema wametoa pikipiki 10 zenye thamani ya milioni 25 kwa Kikundi cha Umoja wa Bodaboda Stendi na kukabidhi vifaa vya viwanda kwa vikundi 7 vyenye thamani ya milioni 92.

Dkt. Pima alisema tangu wa fedha ulipoanza hadi hivi sasa wametoa mikipo ya jumla ya shilingi milioni 584 kwa vikundi 99 ambapo vikundi 44 vya wanawake wamepokea milioni 251, vijana vikundi 36 vimepokea milioni 281 na walemavu vikundi 16 vimepokea milioni 51.5.

Kwa upande wa Waziri Jaffo amezitaka Halmashauri nyingine mfano wa Kaliua katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vijana , walemavu na Wanawake.

Alisema Kaliua imeweza kutoa mikopo ambayo itayasaidia makundi hayo kujipatia kipato na kujiletea maendeleo yao na Taifa.

MWISHO