Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Kisarawe, Mtale Mwampamba,  ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo na Rais John Magufuli walimtimua Chadema kwa makosa ya utovu wa nidhamu mwaka 2013.

“Picha ni DAS wa Kisarawe Mtela Mwampamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo na Rais kwa tuhuma za kutembea na wake za watu,” alindika Mrema katika ukurasa wake wa Twitter.

“Aliyekuwa kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo. Mtela alifukuzwa uanachama wa Chadema na Bavicha kwa makosa ya utovu wa nidhamu 2013,” aliandika Mrema