Hivi sasa tunapoongelea simu, tunaegemea sana kwenye smartphone. Smartphone kwa kiasi kikubwa ni nyepesi kufanya shughuli nyingi ikiwemo shughuli za usalama. Hivyo kwa kutumia uwezo wake huo tutaona jinsi ya kuipata pindi inapopotea au inapoibwa. Lakini pia kama unatumia simu ya kiganjani ya kawaida tutatizama pia jinsi ya kuipata.
Kama simu yako iliyopotea ni ya Apple ningependa ubofye hapa uendelee na Apple moja kwa moja.
Jinsi ya kupata simu iliyopotea: Android:
Simu hizo huwa moja wapo kati ya hizi: TECNO, SAMSUNG SONY, na nyingine nyingi za aina hizi.
Kama simu yako iliyopotea ni android usiwe na wasiwasi. Hebu tufuatilie njia zifuatazo zinazoelezea kwa kina namna gani ya kuweza kuipata simu yako.
>> Kwa kutumia ANDROID DEVICE MANAGER (ADM).
Je, unatumia Google Play Store. Jibu lako bila shaka ni ndio na kama sio basi hakikisha umejiunga na Play Store. Kwa nini nimeanza na hili ni kwa sababu ili kujiunga na Play Store lazima uwe na akaunti ya Gmail. Kwa nini Gmail, kwa sababu hii ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kutambua pahala simu yako ilipo. Android Device Manager ni programu ya google inayopatikana karibu katika kila smartphone ya android. Usijiulize maswali mengi na hata kama haujawahi kuiona usiwaze, hii hufanya kazi ndani ya smartphone yako. Jaribu kuisachi kama usipoipata unaweza kidownload kupitia Play Store au bofya hapa.
Programu hii itatusaidiaje?
ADM hufanya kazi ya kutambua pahala simu yako ilipo kwa wakati husika endapo imeunganishwa na mtandao wa internet. ADM pia huweza kulock au kufuta simu nzima kama umeifanyia settings. Kama simu yako imepotea au imeibiwa fanya yafuatayo ili kuipata.
- Ni rahisi sana. Kama umetimiza yote hapo juu, punde tu unapogundua simu yako imepotea tafuta laptop/computer au simu ya android nyingine yoyote. Sign-in katika gmail kupitia kifaa hicho. Ukisha Sign-In tembelea tovuti ya ADM hapa. Au search tu google 'Android Device Manager' na chagua tovuti yao pale juu kabisa.
- Tovuti hiyo ikishafunguka utaweza kuchagua kifaa chako (Smartphone/Tablet) ambayo imeshajisajili kupitia e-mail yako ya gmail.
- Baada ya kuchagua Google itakuonesha ramani ya wapi simu hiyo ilipo. Baada ya hapo unaweza kuchagua kitufe cha ring. Hata kama aliyeiiba ameshabadili line simu hiyo itaita kwa muda wa dakika kama tano.
- Zaidi pia ni jinsi ya kulock simu yako kupitia huduma hii hii ya ADM. Utaweza kufanya hivyo kwa kuchagua kitufe cha Lock. Kumbuka kitufe hiki kifanya kazi endapo ulifanya settings za kuruhusu ADM kulock na kufuta simu. Faida moja wapo pia ya kutumia option hii ya Lock ni kwamba unaweza kuandika ujumbe ambao yeyote mwenye simu hiyo kwa wakati huo ataiona.
- Pia unaweza kufuta data zote zilizopo katika simu yako hiyo kama unahisi imeibwa au imepotea kabisa kwa kubonyeza kitufe cha Erase.
Njia hii huweza kufanya kazi endapo tu, umeshajiunga na gmail, na pia simu iwe imeunganishwa na internet. Hii ndiyo njia bora kwa mujibu wangu. Usipofanikiwa mara ya kwanza endelea kujaribu usikate tamaa, kama mwizi ameiba smartphone lazima nyakati fulani ataingia tu katika mtandao. Akiingia tu basi kajichanganya. Ni vyema utoe taarifa polisi ni wajibu wao kuhakikisha usalama wako na mali zako.
Kwa kutumia PLAN B
Plan B ni app ambayo imetengenezwa kama suluhisho wa ADM. Plan B inakuwezesha kutambua mahali simu yako ilipo kwa kuinstall programu kupitia mtandao. Hii inakusaidia kama mwanzo haukuwa na ADM na kwa sababu imepotea hauna uwezo wa kudownload na kuinstall. Plan B itakutumia SMS kila baada ya dakika 10 kukupa taarifa juu ya simu yako na mahali ilipo.
Njia nyingine ni pamoja na kutumia apps ambazo itabidi uzi install kabla ya kuibiwa (:))
Apps hizo ni kama hizi zifuatazo:
- Android Lost
- Comodo Mobile Anti-Theft
- Samsung Find My Phone(Kwa watumiaji wa simu za Samsung tu.)
Unaweza kutumia Google Maps pia kufuatilia mwenendo wa simu yako. Kama una akaunti ya Gmail utakuwa tayari umeunganishwa na Google Maps. Tembelea Google Maps kisha nenda katika Settings chagua Location History. Kwa njia hii utaweza kugundua mahali simu yako ilipo.
Je kama simu yangu sio smart kivile?
Kama simu yako ni simu tu ya kawaida ya mawasiliano kama Nokia ya tochi, inapoibiwa au kupotea siyo rahisi kuitafuta kwa njia ya mtandao. Kama unaifahamu IMEI namba, ambayo ni tofauti kwa kila simu unaweza kuiunganisha simu yako hapa katika mtandao wa TrackImei na itaweza kutafuta mahala simu hiyo ilipo pindi itakapo potea.
Asante kwa kusoma hii.