Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohammed Dewji amewahakikishia Wanamsimbazi kuwa hakuna mchezaji yoyote atakaye ondoka ndani ya klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi.

MO DEWJI AWATOA HOFU MASHABIKI WA SIMBA JUU YA USAJIRI WACHEZAJI ...

Katika maelezo hayo kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter, Bosi huyo wa Simba ameongeza kuwa watasajili mchezaji yoyote kutoka klabu yoyote kama tu endapo mwalimu wa kikosi hicho Mbelgiji, Sven Vanderbroeck atamuhitaji.

”Wanasimba wenzangu nataka niwahakikishie hakuna mchezaji wetu yoyote atakaye ondoka SIMBA. Lakini pia tutasajili mchezaji yoyote, kutoka popote. kama mwl wetu atamuhitaji kwenye kikosi chake.. Tutashuka kwa kishindo:hatuna maneno mengi lakini tupo.”- Amesema Mohammed Dewji

Hayo yana jiri baada ya kikosi cha Simba kufanikiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ndani ya siku moja na yote kufaibuka na ushindi mnono katika viwanja vya Mo Simba Arena Bunju.

Katika mchezo wa mapema hapo jana siku ya Jumatatu, ulipigwa asubuhi na Simba akichomoza na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 2 dhidi ya Transit Camp ambayo siku chaache zilizopita ilicheza na Azam FC na kutoka sare ya 0 – 0

MO Dewji muda mchache baada ya wanachama 1216 wa Simba kuridhia ...

Mchezo ulipigwa mchana wa siku hiyo hiyo Simba ikaipiga KMC FC jumla ya magoli 3 -1, wakati vijana hao wa Kinondo juzi iliibuka na ushindi mnono baada ya kuichapa timu ya Wananchi, Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu, Watoto wa Jangwani Young Africans kwa jumla ya mabao 3 – 0.

The post Je Bosi wa Simba, Mo Dewji awatikisa watani wao wajadi  ? ”Tutasajili kutoka popote kocha akihitaji” appeared first on Bongo5.com.