Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz leo ameomba radhi kufuatia mauaji ya mwanaume wa Kipalestina mwenye matatizo ya akili yaliyofanywa na polisi ya Israel.

Israeli defense minister apologizes for unarmed Palestinian's ...

Kuuliwa kwa Iyad Halak mwenye umri wa miaka 32 katika mji wa kale wa Jerusalem jana Jumamosi kumezusha ukosoaji mkubwa na kufufua malalamiko ya muda ya mrefu dhidi ya matumizi ya nguvu ya vikosi vya ulinzi vya Israel.

Gantz ameomba radhi wakati wa kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri akisema wanaungana na familia ya mwanaume huyo kuomboleza na kuahidi uchunguzi wa kisa hicho na hitimisho lake litatolewa.

Ndugu wa Halak wamesema alikuwa kijana mwenye maradhi ya usonji na kwamba alikuwa njiani kuelekea shule ya watu wenye matatizo ya akili pindi alipopiga risasi na kuuwawa. Katika taarifa yake polisi ya Israel imesema ilimshuku Halak kuwa mhalifu baada ya kumuona akiwa amebeba kitu kilichofanana na bastola.

The post Israel yaomba radhi kwa kifo cha kijana mwenye matatizo ya akili appeared first on Bongo5.com.