Ndege za kivita za Israeli zimefanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya kilimo katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kutoka Wizara ya Afya ya Palestina kuhusu mtu kupoteza maisha au kujeruhiwakatika shambulizihilo.

Msemaji wa jeshi la Israeli Avichay Adraee amesema kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya kuwa makombora mawili yalirushwa kutoka Gaza.

Ameendelea kwa kuthibitisha kuwa Israel ilimwaga risasi katika Ukanda wa Gaza.