Wizara ya Afya nchini Kenya kwa mara nyingine imethibitisha idadi kubwa ya maambukizi 123 kwa muda wa saa 24 na kufikisha walioambukizwa kuwa 2,216.

Wizara hiyo imesema kuwa wagonjwa hao wametambuliwa baada ya sampuli 2112 kuchunguzwa.

Naibu waziri wa afya Rashid Aman aMEsema kuwa maambukizi 44 ni jijini Nairobi na 34 huko Mombasa.

Vilevile Kenya imesajili idadi kubwa ya wagonjwa waliopona kwa siku moja baada ya watu 54 kuondoka hospitalini na kufikisha 553 waliopona kufikia sasa,hata hivyo idadi ya waliofariki imefikia 74 baada ya watu 3 zaidi kufariki.