Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetupilia mbali uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa Mahakama hiyo wanaochunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Marekani nchini Afganistan.

"Mkuu (wa ICC) O-Gon Kwon amefutilia mbali hatua zilizochukuliwa dhidi ya ICC," Mahakama ya ICC imebiani katika taarifa, na kuongeza kuwa hatua hizo "zinazuia juhudi zetu za pamoja za kupambana na tabia za kutowaadhibu wahalifu na kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimishwa duniani kote”.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeeleza kuwa, kitendo hicho ni dharau kwa waathirika wa makosa ya uhalifu yaliyofanyika nchini Afganistan.

Vitisho vya utawala wa Trump vimekuepo dhidi ya Mahakama hiyo ya kimataifa tangu mwaka wa 2018. Hata hivyo vitisho hivyo havijazuia uchunguzi kuhusu uhalifu uliofanywa na jeshi la Marekani na shirika la ujasusi la CIA nchini Afghanistan.