IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba leo amerejea kambini na kuungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Simba uliopo maeneo ya Bunju.

Kiungo huyo alisimamishwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kutokana na kuchelewa kuripoti kambini bila kutoa taarifa ambapo wachezaji wenzake waliripoti kambini Mei 27.

Leo Simba imeendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo ratiba rasmi itaanza kutimua vumbi Juni 13.

Simba itaanza kumenyana na Ruvu Shooting ya Masau Bwire Juni 14 Uwanja wa Taifa.