INAELEZWA kuwa miongoni mwa wachezaji watatu ambao wameongezeka uzito ndani ya Klabu ya Yanga ni mshambuliaji wao namba moja David Molinga.

Habari zinaeleza kuwa baada ya vipimo wachezaji watatu wa Yanga wameonekana ni vibonge na wameongezeka uzito ambapo tayari dawa yao imeanza kuandaliwa.

"Wachezaji watatu wameongezeka uzito, Molinga ameongezeka kilo 10 ana kazi ya kupunguza hilo tatizo na pia ana adhabu yake inamhusu kwani ilishakatazwa tangu mapema kwa mchezaji kuongezeka uzito," ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwassa amesema kuwa anatambua kuna wachezaji watatu ambao wameongezeka uzito hao wataandaliwa program maalum.

Molinga, raia wa Congo kibindoni ana mabao nane kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.