Mwakilishi wa jimbo la Mtoni Unguja, Hussein Ibrahimu Makungu (BHAA) amekuwa mgombea wa 22 kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Uris wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.


Bhaa alifika ofisini hapo majira ya saa saba kasoro katika ofisi za chama hicho zilizopo Kisiwandui Mjini Unguja na kukabidhiwa fomu na Katibu wa Kamati Maalumu  ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.


Mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo alishukuru Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuanzisha mchakato ambao upo huru na wa hakli kwa kila mwenye sifa kujotokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ya urais wa Zanzibar.
Pia aliwaomba wananchi kudumish amani na utulivu uliopo nchini katika kipindi cha chote cha uchaguzi Mkuu.