Rais mpya wa Burundi Jenerali Evariste Ndayishimiye anachukua rasmi mamlaka ya urais nchini Burundi leo baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi urais mwezi huu. Lakini je ni changamoto zipi atakazokabiliana nazo kama kiongozi mpya?.

Jenerali Evariste Ndayishimiye anachukua nchi yenye mgawanyiko mkubwa kutoka kwa kiongozi wa zamani Pierre Nkurunziza ambaye alifariki mwezi huu. Nchi ya Burundi inakabiliwa na migawanyiko tofauti, ikiwemo ya ukabila baina ya Watuhu na Watutsi, mgawanyika wa kisiasa baina ya serikali na upinzani. Swali ni je Ndayishimiye atafanikiwa kuitatua migawanyiko hii ambayo ilishindwa kutatuliwa na mtangulizi wake aliyeiongoza Burundi kwa miaka 15?.

Kujumuisha wapinzani serikalini

Evariste Ndayishimiye alipata ushindi kupitia chama tawala cha CNDD-FDD kwa 68.72% ya kura.

Tume ya uchaguzi ilisema kuwa hasimu wake mkuu Agathon Rwasa wa chama (CNL), alipata 24.19% ya kura.

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon RwasaKiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa

Bwana Rwasa aliwasilisha mashtaka mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo, lakini mahakama ya Burundi iliidhinisha ushindi wa Bwana Ndayishimiye

“Tutasahau kipindi kibaya kilichopita ambacho hakistahili kuwa jela yetu, Evariste Ndayishimiye salisema Ndayishimiye wakati wa kampeni za urais nje ya jiji kuu Bujumbura. Aliwahakikishia wafuasi wake kwamba atafanya kila awezavyo kutatua matatizo yanayosababisha mizozo inayolizonga taifa hilo dogo la Afrika Mshariki.

Jenerali Ndayishimiyeatakuwa na kibarua cha kuungana na Rwasa pamoja na wapinzani wengine kutoka vyama vya upinzani vipatavyo 40 kwa kwa ajili ya kuleta umoja na mshikamano wa Warundi wote bila kujali ukabila wala siasa kinyume na mtangulizi wake.

Mzozo wa wakimbizi

Ndayishimiye pia anarithi nchi yenye mzozo mkubwa wa wakimbizi uliosababishwa na vita na ghasia za mauji za muda mrefu nchini Burundi.

Ghasia za kisiasa na kiusalama pamoja na mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na Burundi kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa zimewalazimisha zaidi ya 350,000 kukimbilia nchi jirani na wengine 110,000 ni wakimbizi wa ndani ya nchi.

BurundiWakimbizi wa Burundi

Ndayishimiye hajahusishwa na unyanyasaji wa miaka ya hivi karibuni unaodaiwa kutekelezwa chama cha CNDD-FDD dhidi ya wale wanaoonekana kuwa ni wakasoaji wake. Hata hivyo hakuingilia kati kuzuwia ghasia zilizoikumba Burundi kufuatia uchaguzi wenye utata uliomuweka madarakani mwaka 2015 .

Wakimbizi wa Burundi watasubiri kuona iwapo Meja Ndayishimiye atatoa mazingira salama yatakayowawezesha kurejea na kuishi tena nchini mwao.

Je ni ipi ndoto ya Warundi wanaoishi uhamishoni baada ya kifo cha Rais Pierre Nkurunziza?

Atatakiwa kuwaridhisha majenerali ndani ya CNCC-FDD

Moja ya changamoto kubwa ya urais anayotarajiwa kukabiliana nayo kushughulikia maslahi ya watu binafsi ndani ya chama tawala cha CNDD-FDD. Ushindi wa Ndayishimiye wake umetokana na historia yake ya kijeshi katika CNDD-FDD. Alishinda kwasababu alikua ni mgombea wa chama tawala kwa kupata uungaji mkono wa baadhi ya majenerari wenye usemi ndahi ya chama.

Ikizingatiwa kuwa hakuwa chaguo la mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, kama rais ambaye chaguo lake lilikuwa ni Pascal Nyabenda- Spika wa bunge, itamlazimu Meja Ndayishimiye kuwarai wafuasi wa mtangulizi wake ambao walikua na chaguo la mtu mwingine kwa misingi ya kuepusha mpasuko ndani ya CNDD-FDDS.

Atakabiliwa na changamoto ya kufahamu na kushughulikia maslahi na ushindani tofauti kwa ajilio ya mamlaka na pesa ndani ya chama.

Huenda ikawa vigumu kwa Ndayishimiye kutekeleza sera zake, hususan pale zitakapokuwa kinyume na maslahi ya Majenerali.

Mzozo wa Uchumi

Tangu mwaka 2015, Burundi imeshuhudia kuzorota kwa uchumi. Viwango vya umaskini vimepanda hadi kufikia 74%. Burundi kwa sasa ni nchi ya tatu maskini zaidi duniani.

Ndayishimiye atatakiwa kushughulikia viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na umaskini mkubwa. Wahisani wengi wa kimataifa wamesitisha msaada wao wa Burundi baada ya uchaguzi wa 2015, jambo lililosababisha uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.

Atatakiwa kurejesha uhusiana na mataifa ya Ulaya pamoja na Marekani ambayo yaliiwekea Burundi vikwazo kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofuatia ghasia zilizoibuka wakati na baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2015.

” Ninadhani atatakiwa kutuma ujumbe kwamba anataka kufanya mabadiliko ya kiutawala utawala bora nchini mwake, kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kuheshimu haki za binadamu ..ninamaanisha atatakiwa kuonyesha kuwa anataka kutoa fursa ya kisiasa, uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari. Nafahamu kuwa baada ya kifo cha Nkurunziza itakua ni vigumu kwake kuachana kabisa na mambo aliyoyafanya Nkurunziza mara moja…atatakiwa kufanya mabadiliko haya taratibu. Iwapo atafanya hivyo ninauhakika Muungano wa Ulaya utataka kufanya kazi na yeye naamini. Anasema Filip Reytjens, mtaalamu wa masuala ya maziwa makuu.

Kurejesha mahusiano na nchi jirani

Rais mpya Evaristre Ndayishimiye atatakiwa kurejesha uhusiano mwema na taifa jirani la Rwanda ulioharibika enzi ya mtangulizi wake Pierre Nkurunziza.

Nchi mbili zimekua zikishutumiana kila moja kuhatarisha usalama kwa kuwahifadhi wapinzani wan chi zao.

Rais wa Rwanda Paul KagameRais wa Rwanda Paul Kagame

Licha ya kutegemeana kiuchumi na kuwa na historia zinazofanana, uhusiano wan chi hizi mbili ni wa kihistoria kwani zilikua ni nchi moja kabla ya kutenganishwa na mkoloni.

Baada ya kifo cha Bwana Nkurunziza Rais wa Rwanda Paul Kagame alituma rambirambi kwa Warundi uliokua ni ujumbe wake wa kwanza wa umma kwa nchi hiyo jirani tangu uhusiano wa Rwanda na Burundi ulipoingia dosari mwaka 2015.

Wataalamu wanasema viongozi kutoka nchi hizo mbili sasa wana fursa ya kuboresha mahusiano ya nchi zao na hivyo kuendeleza biashara na matembezi ya raia wan chi hizo ambao wameathirika na uhasama wa viongozi wao.

Chanzo BBC.

The post Hizi ndio changamoto atakazokabiliana nazo Rais mpya wa Burubdi Ndayishimiye appeared first on Bongo5.com.