OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amepanga kumtumia jumlajumla kiungo wake Paul Pogba sambamba na Bruno Fernandes kiungo mpya ambaye aliletwa ndani ya United kuwa mbadala wa Pogba ambaye alikuwa majeruhi.

Pogba atatumika akiwa ni kama namba 10 huku Fernandes akiwa ni kama kiungo mchezeshaji.

Inaelezwa kuwa Pogba kwenye mazoezi amekuwa akichezeshwa kama namba 10 pembeni ya straika na amekuwa akifanya vizuri.

Fernandes amekuwa bora ndani ya United tangu atue kikosini hapo Januari akitokea Klabu ya Sporting na amekuwa ni mchezaji wa kutegemewa akiwa amecheza mechi 5 na kufunga mabao mawili ndani ya United.