SVEN Vandebroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado kwa sasa ni ngumu kuzungumza hali ya kiungo wake Jonas Mkude ambaye aliumia Juni 8, Uwanja wa Simba Mo Arena.

Mkude aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC baada ya kugongana na beki wa KMC dakika ya 53 jambo lililofanya atolewe uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajibu.

Sven amesema:"Kwa sasa ni ngumu kueleza hali halisi ya Mkude kwa kuwa bado hatujapewa vipimo vyake ili kujua ukubwa wa tatizo lake.

"Kinachosubiriwa ni ripoti ndipo tutajua kwamba tatizo lake lipoje na atakuwa imara kurejea uwanjani baada ya muda gani, kikubwa ni kuwa na subira kwa sasa," amesema.

Kikosi cha Simba kinajiandaa na mchezo wa ligi utakaochezwa Juni 14 Uwanja wa Taifa dhidi ya Ruvu Shooting.