Baadhi ya michezo ya Premier League huwenda ikaanza kuonyeshwa bure kupitia mtandao wa kijamii wa You Tube pale msimu wa ligi utakapo anza kurejea tena baada ya lockdown ya janga la virusi vya corona.

Football chiefs want fans to be able to watch every game live when the season resumes

Chini ya pendekezo linaloendelea kujadiliwa hivi sasa, mechi zote 92 zilizosalia zitatangazwa kupitia Sky Sports, BT Sport na YouTube.

Huku mipango iliyopo ni kuhakikisha msimu huo wa ligi unakamilika ndani ya wiki saba pekee, lakini kutokana na michezo hiyo kupigwa pasipo mashabiki, mkurugenzi wa mchezo wa soka amehitaji mashabiki kuwa na nafasi ya kushuhudia kila ‘game’ mubashara.

Katika mipango hiyo, michezo mingi itakuwa ikionyeshwa kupitia Sky Sports na BT Sport ambao wanashikilia haki za matangazo.

Mtandao wa You Tube upo katika mazungumzo ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kurusha matangazo hayo bure, yakiwa mubashara.

Mara ya mwisho kwa mechi za Premier League kuonyeshwa bure ilikuwa ni msimu wa mwaka 2013-14, siku hiyo Sky Sports iliweza kurusha bure mchezo wa Manchester United dhidi ya Swansea, wakati Crystal Palace ikiwakabili Arsenal.

The post ‘Game’ za Premier League kuonyeshwa bure You Tube  appeared first on Bongo5.com.