Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amejeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Dodoma.

Taarifa rasmi za awali kutoka kwa ndani ya Chadema na kwa watu wa karibu wa Mbowe zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea wakati kiongozi huyo akirejea nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo Mbowe amelazwa katika hospitali moja mjini Dodoma akiendelea na matibabu huku mguu wake mmoja ukiwa umevunjika.