KLABU ya Yanga imeanza kutesti mitambo yake kwanza kabla ya kukutaa na Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Juni 13 Uwanja wa Kambarage.

Mechi mazoezi ya kwanza, Yanga wameshinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Transit Camp inayomilikiwa na Jeshi.

Mechi hiyo ya kirafiki imechezwa kwenye Uwanja wa Chuo Cha Sheria jijini Dar es Salaam, jana.


Mabao ya Yanga yalipachikwa kimiani na Bernard Morrison, Feisal Toto na Mrisho Ngassa.


Jumapili wana kibarua kingine tena cha kumenyana na KMC mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.