Kisiwa cha Ilha de Queimada Grande kipo maili 90 hivi kutoka kwenye jiji la São Paulo nchini Brazil, huko inakadiriwa kuwa wapo nyoka 2,000 wanaoishi katika kisiwa hicho chenye ukubwa wa mita za mraba 430,000 na inaelezwa kuwa kuna nyoka mmoja kila unapokaribia kumaliza mita za mraba moja hadi tano.

Kwenye kisiwa hicho ndipo anakopatikana pekee mmoja wa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, Golden Lancehead Viper.

Wataalamu wanasema sumu ya nyoka huyo ina nguvu karibu mara tano ya nyoka yeyote anayepatikana duniani kiasi cha kuweza kuyeyusha nyama ya mwili wa mwanadamu.