Wiki iliyopita pia tovuti ya habari ya Axius ilivinukuu vyanzo vya kuaminika vikisema kuwa kitabu hicho chenye utata cha Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani, kitafichua habari zaidi kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Trump katika White House, mbali na kadhia ya Ukraine Gate.
Gazeti la Washington Post limesema limepata maelezo zaidi kutoka kwenye kitabu hicho cha Bolton kuhusiana na kashfa ya hivi karibuni ya Trump kuhusu ombi lake kwa China ili imsaidie kushinda uchaguzi.
Ni kutokana na kashafa hiyo ndipo Trump na maafisa wake wakafanya kila jambo ili kujaribu kusimamisha uchapishwaji wa kitabu hicho