Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kanda ya Kati na Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Mizengo Pinda ameitaka Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ya Chama hicho, kuhakikisha hakuna mgombea wa (CCM) anapatikana kwa kutumia fedha. "Usikubali kutumia fedha kama sehemu ya kuvuta hisia ila upigiwe kura, ni mtihani mkubwa lakini itabidi tuusimamie, Bwana mkubwa anajua atakachokifanya lakini inaelekea tutakuwa nakautaratibu kagumu kidogo" alisema Bw. Pinda.

Bw. Pinda amelitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma, ili kujua hali ya siasa mkoani humo, wakiwa wameanzia ziara hiyo katika wilaya ya Chamwino