Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege) amezidiwa ghafla akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko kwa matibabu

Bwege, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na viongozi wengine 6 wa ACT Wazalendo walikamatwa na Polisi leo asubuhi wakiwa katika mkutano wa ndani wa chama Wilayani Kilwa

Maelezo ya awali ya Polisi yamewataka Viongozi hao kuwa na Wadhamini 8, kila mdhamini atamdhamini Kiongozi mmoja ila kwa mujibu wa ACT, Viongozi wa Kituo kwa sasa wameondoka wakidai kuwa na kikao na Mkuu wa Wilaya

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amesema aliagiza Polisi wawakamate Viongozi kwa sababu wamefanya maandamano bila kibali na kulikuwa na fujo kwa umma ikiwemo milio ya honi