Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza unazikwa leo kwenye makaburi ya mji wa Gitega mji mkuu wa kisiasa ulioko katikati mwa Burundi 

Hafla ya mazishi zinatarajiwa kuongozwa na rais mpya jenerali Evariste Ndayishimiye na wakuu wengine wa serikali. 

Kwa mjibu wa tangazo lililotolewa na serikali ya Burundi, hafla itaanzia kwenye 'hospital du Cenquantenaire Twese Turashoboye' iliyoko kwenye mkoa wa Karusi ambako mwili wake umehifadhiwa. 

Wananchi wametakiwa kusimama kwenye barabara kumuaga marehemu.
OPEN IN BROWSER