Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapenda kuwataarifu umma wa Watanzania kupitia Mkutano huu kuwa jumla ya Wanachama 3, wamejitokeza kutia nia kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za Udiwani, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao itatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii, kwa vyombo vya habari, wamejitokeza ndani ya muda uliowekwa kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa kutangaza kusudio la kuwania Nafasi za Uongozi kwenye Vyombo
vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinataamka; “Kwa Nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa taarifa zinazofuata.”

Mtakumbukwa mnamo Juni 06, mwa huu, Ofisi kuu ya Chadema Zanzibar kupitia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe Salum Mwalimu alifungua rasmi milango kwa mwanachama yoyote anaye taka kutia nia nafasi ya Urais, kuandika barua ya kusudio lake kwa Katibu Mkuu.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

1. Hashim Juma Issa
2. Mohamed Ayoub Haji
3. Said Issa Mohamed

Aidha mwanachama mmoja ametia nia kwa njia ya simu. Hata hivyo kwa kuwa bado hajakamilisha baadhi ya taratibu kwa sasa hatutataja jina lake.

Chama kitatoa utaratibu utakao fuata baada ya kukamilisha taratibu za ndani ya Chama. Kwasasa watia nia wote hawa wanapaswa kuendelea
kuzingatia taratibu za chama mda wote.

Hata hivyo, Chama kinawakubusha wanachama wake kuwa kushindwa kutangaza nia hakumnyimi mwanachama kushiriki mchakato huu katika hatua za uchukuaji fomu.