UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna mchezaji yoyote anayeweza kuondoka kwa sasa ndani ya Simba na kuibukia Klabu yoyote kwa sasa iwapo atakuwa anahitajika ndani ya timu.

Hivi karibuni ilikuwa ikielezwa kuwa watani zao wa jadi Yanga walikuwa kwenye hesabu za kusepa na saini ya Deo Kanda, Clatous Chama na Said Ndemla.

Kupitia Ukurasa wao rasmi wa Instagram, Simba imeripoti taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewiji,' MO' ikisema:-"Wanasimba wenzagu, nataka niwahakikishie hakuna mchezaji wetu yoyote atakayeondoka Simba.

"Lakinipia tutasajili mchezaji yoyote kutoka popote kama mwalimu atamuhitaji kwenye kikosi chake. Tutashuka kwa kishindo. Hatuna maneno mengi lakini tupo."