Rais Magufuli ametangaza kufungua shule zote  nchini na shughuli zingine za kijamii zilizokuwa zimesitishwa kisa ugonjwa wa Corona

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne June 16, 2020 wakati akilihutubia Bunge kabla ya kulifunga ili kupisha mchakato wa uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Octoba Mwaka huu

Amesema hali ya Corona nchini inaendelea vizuri na imepungua sana

“Kutokana na mwendendo wa corona kuendelea kuwa mzuri, corona imepungua sana, naomba nitangaze kuanzia June 29 mwaka huu nafikiri itakuwa Jumatatu, shule zote zilizokuwa zimebaki zifunguliwe, lakini Watanzania waendelee kuchukua tahadhari”-Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli  amesema shughuli nyingine zote kama kufunga ndoa nazo ziendelee na maisha lazima yarudi kama ilivyokuwa awali