Kupitia katika ukurasa wake wa Instagram Majizo ameandika hivi”Nimekuwa kwenye hii tasnia kwa miaka mingi, natambua na kuheshimu mchango wa watu na tasisi zote zilizohusika kutufikisha hapa.

Lakini majira yanabadilika, na kila siku tunahitaji kuongeza nguvu. Kwa sasa nafahamu kwamba @efmtanzania na @tvetanzania, tunaangaliwa sana na vijana kwamba tutaipeleka hii tasnia katika muelekeo wanaotaka. Katika safari hii tunaalika watu wote ambao tunaamini wataunda jeshi imara.
.
Hakuna haja ya kueleza kuhusu uwezo na mchango wa Hamisi Mandi @bdozen kwenye hii tasnia. Ni furaha yangu kutangaza kwenu kwamba #Twangala amejiunga na @efmtanzania na @tvetanzania

#DozenAmetua

 

https://bit.ly/3duoLij

The post Breaking: Majizo athibitisha B Dozen rasmi amejiunga na Efm – Video appeared first on Bongo5.com.