Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi la Clock Tower, Kenyatta, Bank House na Madaraka wameungana
na wananchi wengine kuadhimisha Wiki ya Maziwa hapa nchini inayohamasisha matumizi zaidi ya
unywaji wa maziwa.
Katika tukio hilo, wafanyakazi walipata nafasi ya kunywa maziwa na mazao mengine yatokanayo na
maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Kilimanjaro Fresh na Tanga Fresh huku wakizingatia kanuni zote
za kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona.

NMB Bank House

NMB Clock Tower

NMB Kenyatta

NMB Madaraka.

Meneja Uhusiano Mwandamizi wa NMB Kanda ya Kaskazini anayeshughulikia Kilimo- Oscar
Rwechungura alisema katika kuadhimisha Wiki ya Maziwa kwa kushirikiana na wadau wengine katika
sekta ya maziwa wanawezesha sekta hiyo katika mnyororo wa thamani.
“NMB inawezesha sekta hii kuanzia ngazi ya mwanzo kwa wafugaji wenyewe, wafanyabiashara wa
dawa za mifugo na wasindikaji wa mazao ya maziwa katika kuhakikisha tunaimarisha sekta nzima ya
maziwa na kuimarisha afya za watumiaji wakiwemo wafanyakazi wa NMB,” alisema Rwechungura

Alisema lengo la NMB ni kupanua wigo kwa wafugaji wadogo ili waweze kupata huduma za kifedha kwa
njia rahisi ili kuongeza idadi ya ng’ombe, vyakula vya mifugo na huduma za matibabu ya mifugo ili
kuongeza tija ya ufugaji wao.
“Lengo letu ni kuwawezesha wazalishaji wa maziwa kuongeza tija,badala ya mfugaji kutegemea
kupata maziwa lita mbili kwa siku jambo ambalo halimfanyi aone faida ya kazi anayoifanya
tunatamani apate lita 20 na zaidi kwa siku hivyo ili mfugaji apate faida lazima aongeze matumizi kwa
kupata uwezeshwaji kutoka kwetu,”
NMB haishii kuwawezesha wafugaji wadogo na kati kupata mitaji pekee bali inawaunganisha na masoko
ili kuwezesha mnyororo wa thamani katika sekta nzima ya maziwa kuanzia kwa mfugaji hadi
anayepeleka maziwa sokoni.

The post Benki ya NMB yaadhimisha Wiki ya Maziwa appeared first on Bongo5.com.