Amiri kilagalila
Baraza la Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe lililoketi Juni 20/2020 chini ya Katibu wake wa Mkoa Ndg, Hussein Mwaikambo (Senetor) pamoja na mambo mengine kwa kauli moja lilipitisha Azimio la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa Utendaji wake uliotukuka.

Akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Njombe Ndg, Hussein Mwaikambo Katibu wa Jumuiya hiyo alisema, katika Kipindi cha Miaka mitano Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuliongoza Taifa na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake hivyo Baraza linampongeza.

“Mhe, Rais na Mwenyekiti wetu wa Chama amefanya kazi kubwa na yenye heshima ndani ya Chama na Jumuiya zake, Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Njombe tunampongeza kwa hilo pia tunaahidi kuendelea kumuunga mkono, zoezi hili la kumdhamini kupitia Fomu ya kugombea Urais sisi Jumuiya ya Wazazi tumelifanya” Alisema Mwaikambo.

Aliongeza kuwa Dkt, Magufuli Baada ya kupitishwa rasmi na Chama kwenda kugombea nafasi ya Rais akishindana na vyama vingine Jumuiya hiyo itahakikisha inatoa mchango wa Fedha ili Mgombea aweze kuchukua Fomu ya Serikali tayari kwa ushindi ili aendelee kuwatumikia Watanzania.

Bw, Imani Fute Mjumbe wa Baraza la Wazazi CCM Mkoa wa Njombe alitoa Wito kwa Wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha wanatimiza Majukumu yao kama Wazazi ya kuendelea kuwalea na kuwaelimisha Vijana ambao wanalengo la kuwania nafasi za Uongozi kuhakikisha wanazingatia Kanuni, Miongozo na Katiba ya Chama.

“Huu ni Mwaka wa Uchaguzi yapo mengi ambayo yanaendelea kufanyika huko kwenye Kata na Wilaya zetu sisi kama Wazazi tuhakikishe tunawaelimisha Vijana wetu wazingatie Kanuni na Katiba ya Chama ili wapite kwenye njia sahihi na kufanikisha malengo yao ya kuwa Viongozi kupitia CCM” Alisema Fute.

Aidha Mjumbe wa Baraza hilo Ndg, Nathanael Maxona na Wajumbe wengine kutoka Wilaya za Njombe, Ludewa, Makete na Wanging’ombe walishiriki Baraza hilo na kupokea Maelekezo tayari kwa Utekelezaji ili kutafuta Ushindi wa Chama kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.