Msanii Barakah The Prince amekiri kusema staa wa BongoFleva Alikiba ni msanii mkubwa pia lazima ujipange ili uweze kufanya naye kazi.

Barakah ambaye alikuwa anatofauti za masuala ya kazi na uongozi wa Alikiba siku za nyuma, amesema kwa sasa yupo tayari kufanya naye kazi na akihitaji atawasiliana na menejmenti yake ili waweze kufanikisha.

"Mimi na Alikiba hatujakuatana, hatujaongea na hatujawasiliana kwa muda mrefu kwa sababu kila mtu ana mishe mishe zake, sina namba zake na sidhani kama utamuuliza yeye kama atakuwa na namba zangu ila mimi namchukulia kama kaka yangu, natamani kufanya naye kazi ikitokea nipo tayari nitaiambia menejmenti yake wakikubali tutafanya" ameeleza Barakah The Prince

Wawili hao wameshafanya kwa pamoja ambayo ilifanya vizuri kwenye chati za muziki Bongo, mwaka 2016 iitwayo nisamehe kipindi hicho Barakah yupo katika lebo ya Rockstar ambayo  Alikiba alikuwa na shea zake.