SALVATORY NTANDU
Mkamo wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Idd amewataka viongozi wa ngazi za matawi,kata,wilaya na Mikoa kuzipokea fedha zinazotolewa na baadhi ya watia nia wanaotaka uongozi ndani ya Chama cha mapinduzi(CCM) mkoani shinyanga na kuwafichua kwa vyombo vya usalama ili wachukuliwe hatua Kali za kisheria.

Kauli hiyo ameitoa Julai 26 mwaka huu wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo akiwa ni mlezi wa CCM mkoani humo baada ya kupokea taarifa ya chama kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alisema kuwa kiongozi anayenunua kura hafai kuwemo ndani ya CCM mpya inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Maguli kwani atatanguliza mbele Maslahi yake binafsi pindi atakapochaguliwa.

"Wapo wapambe wa wagombea wameanza kuunguka katika matawi na kata na  kugawa shilingi elfu 5000 hadi elfu 20000 zipokeeni lakini msiwachague kwa sababu CCM inautaratibu wake wa kuwapata viongozi,"Alisema Balozi Idd

Aliongeza kuwa CCM haitapitisha jina la Mgombea yeyote atakayebainika kutoa fedha ili kupata nafasi ya kuchaguliwa hata kama atakuwa amepitishwa na mikutano mikuu ndani ya Chama ili kutokomeza vitendo vya rushwa nyakati za uchaguzi.

"Vyombo vyetu vya dola vimejipanga kikamifu kudhibiti vitendo vya rushwa ambavyo husababisha wagombea wasiokuwa na sifa kuchaguliwa ambao sio chaguo la wananchi na kuwakosesha watu wenye sifa kuchaguliwa,"alisema Balozi Idd.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Gaspar Kileo ambae pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa (NEC)aliwataka makatibu wa matawi,kata, na wilaya kuwachukulia hatua Kali watia nia ambao watakaobainika kuanza kampeni kabla ya Muda wao.

"Wakamateni ili vyombo vyetu viwafanyie kazi kwa kutoa rushwa halafu wakija kwenye chama sisi hatutapitisha majina yao,"alisema Kileo.

Kuanzia tarehe 7 mwaka huu hadi 14 mchakato wa uchukuaji wa fomu ndani ya CCM utaanzaa ambapo kwa sasa watu wote wanaotaka kugombea nafasi za ubunge na udiwani kutoruhusiwa kufanya kampeni.

Mwisho.